Elizabeth Micheal
Elizabeth Micheal

Famous Tanzanian actress Elizabeth Michael has penned a love message for her second born child, Gracious.

Michael who is married to media mogul Majizzo announced the arrival of the child on Christmas day.

She has now shared with her fans a letter to her daughter who she refers to as God's grace for her.

 

Dear G,

Ni kwa NEEMA ya MUNGU tumekutana hapa DUNIANI nikiwa kama MZAZI wako,yaani mtu NILIYEAMINIWA na MUNGU kulitunza KUSUDI LAKE aliloweka NDANI YAKO mpaka pale utakapopata UWEZO/FAHAMU za kuendelea kufanya hivyo wewe wenyewe….!

Ningependa ujue NEEMA Hii iliyotukutanisha ndio imekuwa KIUNGO KIKUU kwenye maisha yote ya huyu mzazi wako.*

 

NEEMA YA MUNGU ilinipitisha palipoonekana HAPAWEZEKANI kupita .

*NEEMA YA MUNGU ilinipa MWANZO katika nyakati zilizoonekana kama ndio mwisho kwangu.

*NEEMA YA MUNGU imeniwezesha KUMILIKI vitu ambavyo vilikuwa kama NDOTO tu kwenye maisha yangu.

*NEEMA YA MUNGU imeniweka kwenye NAFASI ambazo kibinadamu naonekana sikustahili au hata sasa sistahili kuwepo…ila Ndo hivyo nipo 😀

*NEEMA YA MUNGU imeniketisha na WAKUU mwanangu…ambao sikudhani kama ingewezekana mimi kuwa sehemu yao.Na hayo ni machache tu katika meeengi ila kwa ufupi

NEEMA YA MUNGU Ndio MAISHA YANGU,hakuna niliyowahi kuyafanya au ninayoyafanya hata leo hii kwa UJANJA wangu au AKILI yangu ya kibinadamu pekee…Jinsi nilivyo,mahali nilipo,nilivyonavyo na mengine yote

NI KWA NEEMA TU.Na haya ni MAOMBI na MATAMANIO yangu…

NEEMA YA MUNGU ISIKUACHE WALA KUKUPUNGUKIA katika siku zote za maisha yako hapa duniani.Wewe ni MWANADAMU hautakuwa mkamilifu….utakosea,utaanguka n.kLakini mara zote na katika yote

NEEMA YA MUNGU ISIKUACHE na IKUONGOZE kwenye KUSUDI LAKE TU..!Muonekano,Uwezo wa Kifikra au Mali na karama nyingine nyingi UTAKAZOBARIKIWA na MUNGU vyote viwe ZIADA yako tu…Lakini

NEEMA na KIBALI CHAKE vikutangulie KWANZA katika YOTE…maana ndani NEEMA na KIBALI utapata vingine VYOTE (mimi ni shahidi wa hili)🙏

Nasimama kwenye neno la MUNGU (Kumbukumbu la Torati 32:1) MBINGU na ARDHI Ziandike maneno haya yote NINAYOYAKIRI kwa mdomo na vidole vyangu….Na YAKATIMIE KWAKO sawasawa na MAPENZI YA MUNGU🙏Wewe ni MWENYE NEEMA BINTI YANGU…Na hilo ndilo jina lako.!🙏

Her Name is GRACIOUS (MWENYE NEEMA )

❤️With Love,

Mama GG.